Nilianza na Kuku 8 wa Kienyeji, Lakini Nimezalisha Kuku wa Kienyeji 300

Описание к видео Nilianza na Kuku 8 wa Kienyeji, Lakini Nimezalisha Kuku wa Kienyeji 300

Nilianza na Kuku 8 wa Kienyeji, Lakini Nimezalisha Kuku wa Kienyeji 300 ‪@changamkiafursa‬

Katika mfululizo wa vipindi vyetu vya ufugaji wa kuku hapa changamkiafursa, tunahitaji kumuinua mfugaji wa kuku wa kienyeji aache kufuga kuku kwa mazoea na aanze kufuga kuku wa kienyeji kibiashara.
Ili ufuge kuku wa kienyeji kibiashara unatakiwa kuwa na makoo yasiyopungua 250 na sio rahisi kwa Wafugaji wa kuku wa kienyeji kuwa na mtaji mkubwa kiasi hicho.

Sehemu 1:    • NJIA RAHISI YA KUPATA VIFARANGA WENGI...  

Sasa ili kulikamilisha hilo mfugaji anapaswa kuwa na uwezo wa kuzalisha vifaranga wengi wa kienyeji kwa pamoja, ambavyo vitampa mfugaji hamasa ya kuweka nguvu kubwa kwenye uleaji vifaranga kitu ambacho kitachangia ongezeko kubwa la idadi ya kuku wa kienyeji na kuleta tija kibiashara.

Kufanikisha zoezi hili mfugaji anapaswa kuandaa vitu vifuatavyo:-
1. Banda bora na litakalo endana na idadi ya kuku anaohitaji kufuga.
2. Makoo na jogoo (Makoo ni kuku ambao wametaga angalau mara moja). Makoo watasaidia kupunguza muda wa kusubiri ili kuliona yai la kwanza.
3. Vifaa vya maji, chakula na Chumba maalumu cha kulelea vifaranga
4. Makasha au box la kutunzia mayai
5. Elimu ya ufugaji bora wa kuku, itasaidia kutatua changamoto mbalimbali za mradi wako

Baada ya kukamilisha maandalizi hayo, sasa twende tukaanze kuzihesabu hatua za awali za kufata ili kukusanya vifaranga wengi kwa pamoja na baadae uleaji wa hao vifaranga watakaokuwa kuku wa baadae.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке