Msikilize Mwamposa (Bulldozer)

Описание к видео Msikilize Mwamposa (Bulldozer)

Kampeni ya mabadiliko ya tabia kuhusu tahadhari ya ugonjwa wa Homa kali ya mapafu (COVID19) inaendelea sehemu mbalimbali za Tanzania ikiwa ni sehemu ya mkakati maalum wa kufikisha ujumbe kwa watanzania. Huu ni mkakati ulioanzishwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kushirikisha wadau mbalimbali. Kikosi kazi cha WASH kinaongozwa na Ndugu Anyitike Mwakitalima, Mkuu wa Kitengo cha Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mshehereshaji Mkuu katika kikosi hiki ni Ndugu Mrisho Mpoto, msanii nguli wa nyimbo za mashairi ambaye ni Balozi wa Kampeni ya Nyumba Ni Choo. Pia yupo mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania kutoka Kamisheni ya Ushirikishwaji Jamii, Stafu Sajenti Valentino Ngowi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке