Wakaazi wafunga barabara kuu ya Emali-Loitokitok kufuatia mzozo wa shamba

Описание к видео Wakaazi wafunga barabara kuu ya Emali-Loitokitok kufuatia mzozo wa shamba

Shughuli za Uchukuzi kwenye barabara kuu ya Emali-Loitokitok katika eneo la Imbirikani kaunti ya Kajiado zilitatizika pakubwa baada ya wakazi kufunga barabara hiyo kwa zaidi ya saa sita. Wakazi hao wanalalamika kuwa Maafisa wa Serikali wameingilia mzozo unaozingira uongozi wa shamba la Imbirikani ambapo kesi kuhusu mzozo huo ingali mahakamani. Wasafiri, wakiwemo watalii waliokuwa wakiingia na kutoka kwenye mbuga ya Amboseli walijipata kwenye patashika hiyo na kulazimika kukaa barabarani kwa muda mrefu. Robert Masai anaarifu zaidi kutoka Kajiado.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке