Mbowe: Chadema tunatamani wakati wote nchi iongozwe na Katiba

Описание к видео Mbowe: Chadema tunatamani wakati wote nchi iongozwe na Katiba

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema chama hicho kinatamani wakati wote nchi iongozwe na katiba iliyo bora ili kutengeneza ustawi ulio bora kwa wananchi wote.
“Tunaamini katiba iliyo bora itazaa sheria bora na vyote kwa pamoja vitatengeneza ustawi uliobora kwa raia wote. Nayazungumza haya nikiamini kwa muda mrefu katika nchi yetu kumekuwa na utamaduni wa walioko katika madaraka kuamini utashi wa kiongozi mkuu ndiyo unapaswa kuwa Dira ya Taifa.
“Dira ya Taifa letu wakati wote ili iwe ya haki kwa makundi na watu wote haipaswi kuwa utashi wa kiongozi mkuu, inapaswa kuwa imechimbiwa kwenye katiba ya nchi.
Mbowe ametoa kauli hiyo leo Septemba 19, 2024 jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) uliowakutanisha wadau kujadili tathimini ya hali ya demokrasia nchini.
Imeandikwa na Faraja Masinde

Комментарии

Информация по комментариям в разработке