MWAITEGE: SIJAFA MIMI NI MZIMA WA AFYA NJEMA

Описание к видео MWAITEGE: SIJAFA MIMI NI MZIMA WA AFYA NJEMA

Muimbaji wa nyimbo za Injili, ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Safina, Bonny Mwaitege @bony_mwaitege amesema yeye ni mzima wa afya njema na ameshangazwa na taarifa zinazomzushia kifo.

Akizungumza nami kwa njia ya simu amesema kuwa anamshukuru MUNGU yeye ni mzima wa afya na watu watulie tu.

"Ninamshukuru MUNGU kwamba niko mzima wa afya na sijapata tatizo lolote kwa neema ya Bwana". Alisema Mwaitege

Ameongeza kwa kuwapa pole wale wote walioshitushwa na taarifa hizo za uzushi na kuwataka watulie.

"Ninaomba watu wale ambao wamepata mshituko, kwamba watulie tu MUNGU wetu anahitaji tumtumikie". Aliongeza Mwaitege

Комментарии

Информация по комментариям в разработке