SITA WADAKWA KWA TUHUMA ZA KUWACHOMA MOTO WATATU TANGA, YUMO MFANYABIASHARA

Описание к видео SITA WADAKWA KWA TUHUMA ZA KUWACHOMA MOTO WATATU TANGA, YUMO MFANYABIASHARA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linawashikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya watu watatu yaliyotokea Septemba 23, 2024, ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Korogwe, kijiji cha Sindeni, wilaya ya Handeni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 2, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, amesema kufuatia tukio hilo, jeshi hilo limefanya uchunguzi wa kina pamoja na msako uliowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Mchunguzi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Benard Kizughuto (31), mkulima kutoka Msambiazi, Korogwe; Marko Jambia (28), mkulima kutoka Lushoto; Peter Jambia (31), mkulima kutoka Msambiazi, Korogwe; Hassani Kitombo (53), mkulima kutoka Kwamaraho, Handeni; Jamesi Mkama, maarufu kama "Teacher" (42), mfanyabiashara kutoka Mtonga, Korogwe; na Omary Salehe (20), mkulima kutoka Kwamaraho, Handeni.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo, huku watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi wakisubiri hatua za kisheria. Kamanda Mchunguzi aliahidi kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.
(Imeandikwa na Rajabu Athumani)

Комментарии

Информация по комментариям в разработке