Mzee Kilomoni: Simba Kuna Matatizo, 'Watu Wamevamia Klabu'

Описание к видео Mzee Kilomoni: Simba Kuna Matatizo, 'Watu Wamevamia Klabu'

Subscribes:   / kidanistars  
MWANACHAMA wa klabu ya Simba, Hamis Kilomoni amesema kamwe hawezi kung'oka ndani ya klabu hiyo mpaka pale katiba itakapofuatwa huku akimtaka Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Crescentius Magori kuacha kupambana naye .


Alisema tangu mwaka 2014 Simba ilipokuwa chini ya Rais Evans Aveva walijaribu kumtoa katika nafasi hiyo lakini haikuwezekana kutokana na kushindwa kufuata katiba sasa anashangazwa na Magori kuendelea kupambana naye.


"Magori sio kiongozi halali katika klabu ya Simba amechaguliwa na mtu mmoja mimi nimepitishwa na mkutano mkuu wa klabu sasa nakubali vipi kuondolewa na mtu ambaye amewekwa tu madarakani na mtu mmoja,"

"Sina sababu ya kuendelea kung'ang'ania madaraka endapo sheria zitafuata kwa sababu kwanza naomba kufahamu baada ya mimi kuondolewa madarakani hao wanaoingia kuziba nafasi wamepitishwa kwa kufuata sheria?," alihoji.

"Kama Aveva alishindwa Magori ni nani hadi apambane na mimi kuniondoa madarakani na sielewi ni kwanini wanapambana kunitoa madarakani lazima kutakuwa kuna kitu kinatafutwa siwe,i kukubali," alisema.


Instagram:   / kidanistars  

Facebook:   / kidanistars  

Twitter:   / kidanistars  

Комментарии

Информация по комментариям в разработке