Dizasta Vina - Not A Hero

Описание к видео Dizasta Vina - Not A Hero

Official Lyrics Video for Tanzanian hip hop artist, songwriter, and record producer Dizasta Vina, Performing a record 'Not A Hero' Off the Album 'A father Figure'

Stream/Download Not A Hero
Boomplay - https://www.boomplay.com/songs/188023113
Audiomack - https://audiomack.com/dizastavina/son...
Mdundo - https://mdundo.com/song/3324764
Spotify - https://open.spotify.com/album/7it4TZ...
Apple music -   / not-a-hero-single  

Lyrics
Nikiwa narudi kutoka kwenye sherehe za mahafali
Nikakatiza kwenye mtaa wenye taa mbali
Kwahiyo giza kubwa nikiwa na tahadhari
Huku nikitafakari

Vipi maisha yatakuwa? shule nimeua naingia mtaani
Je nitapata kazi au nitalamba nyasi?
Au nitaingia shambani ama nitaishika gun?
Mawazo kichwani kama nitaipata mali

Mbele namwona Lily, tunaenda njia moja
Maana tunakaa mtaa mmoja, Just kona mbili
Bado alikuwa amevaa joho la kuhitimu
Na mkononi simu, akibofya nini..

Alitembea kulia kushoto, mwendo wa madaha
Sometimes aruke kidogo kuonyesha furaha
Aliyapiga majani kwa fimbo
Nilisikia sauti kwa mbali akiimba wimbo

Nilitamani kumwita niliogopa
Nilibaki nyuma nilizuga sikumkaribia
Maana Kitambo ninamjua ila daily tu navunga
Vile mazoea hatuna na namfagilia

Haikutokea siku, nidiriki kuthubutu hata
Kumfata kumwomba contacts,
Japo tunajuana tulisoma sekondari,
Msingi na vidudu kumfuata niliona woga

Moyoni napiga kelele "Come and save me"
Nazama kwenye bahari hii ya mapenzi
Pengine pia alinihusudu ila sikuwa kamili
Pengine nilikuwa na nguvu ila sikuwa jasiri

Aligundua kuwa, namfata kwa nyuma
Aligeuka aliniangalia nikauchuna
Alinipungia mkono niliupunga pia
Lakini bado nilivunga sikumkaribia

Hofu iliufunika upendo wangu
Kila nikimwaza yeye niliiwaza kesho yangu
NIlitamani mrembo asimame nimsemeshe soga
Labda mikono tushikane tutembee pamoja

Alikuwa karibu pia alikuwa mbali
Nilijua kuwa naye penzini ingekuwa zali
Nilitamani kumfata nimweleza nilichowaza
Nilishindwa 'cause...

(I'm not a Superhero)
Ile haikuwa filamu so, I was not (a Hero)
Ushujaa ni dhahania uhalisia hauna (Hero)
(Yeah yeah yeah, I'm not a Superhero)
(Yeah yeah yeah)

Alitembea mbele nilibaki nyuma
Mimi na moyo wangu mpweke uliojaa ufa
Nikifurahia jinsi asili ilivyomuumba
Nikijua dhahiri hofu haitazaa tunda

Niki-fantasize siku atakuwa wangu
Nikiomba mizimu ya mapenzi isikie dua zangu
Na baridi ilinipiga ila haikufua dafu
Nilikuwa mkavu

Nilizidiwa na mawazo hisia nilikuwa nazo moyoni tele
Masomo tumemaliza nitakuwa simwoni daily
Mawazo nilipoyarudisha ndipo hofu ikanishika
Niligundua Malaika yule simwoni mbele

Sikusogea karibu nilishapagawa
Hisia ziliniambia kuna kitu hakikuwa sawa
Nikasikia purukushani nikaingiwa hofu
Nikavamia Karakana chini ya gari bovu

Nikajificha

Nikaona vijana wamefura dhambi
Mkononi mapanga usoni wamekula Maski
Wakamwingiza Lily kwenye karakana
Hawamkumvua nguo zake walizichanachana

Nilimwona Lily, Lily aliniona mimi
Tukagonganisha Macho ila sikutoka chini
Akijua kuwa nina mpango wa kumsaidia
Niliogopa nikamvungia akaanza kulia

Maninja walimbaka mmoja mmoja
Wakigombea kuanza hawakutaka ngoja ngoja
NIlitamani muda urudi nimsemeshe soga
Labda asingevamiwa kama tungekuwa pamoja

Akipiga kelele "Come and save me"
Sauti yangu hata kutoka tu haiwezi
Pengine yale yalinihusu ila sikuwa kamili
Pengine nilikuwa na nguvu ila sikuwa jasiri

Alininyooshea mkono sikuunyoosha pia
Alitamani nitoke niende kusaidia
Hofu iliufunika upendo wangu
Nilipoyaona mapanga niliiwaza kesho yangu

Alikuwa karibu, ila alikuwa mbali
Kutoka kumwokoa pengine ingekuwa zali
Nilitamani kumfata nimwondoe kwenye mkasa
Nilishindwa 'cause

(I'm not a Superhero)
Ile haikuwa filamu so, I was not (a Hero)
Ushujaa ni dhahania uhalisia hauna (Hero)
(Yeah yeah yeah, I'm not a Superhero)
(Yeah yeah yeah)

Комментарии

Информация по комментариям в разработке