Madhara ya Hofu ya Mabadiliko | Rev. Dr. Eliona Kimaro

Описание к видео Madhara ya Hofu ya Mabadiliko | Rev. Dr. Eliona Kimaro

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY (FRIDAY PRAYERS) 12/ 07/ 2024

SEMINA YA NENO LA MUNGU:
MADA:
"HOFU YA MABADILIKO"
(FEAR OF CHANGE)

SOMO LA LEO:
MADHARA YA HOFU YA MABADILIKO
Kutoka 15 : 10 - 27

NENO KUU:
"UTABARIKIWA UINGIAPO, UTABARIKIWA NA UTOKAPO"
KUMBUKUMBU LA TORATI 28 : 6
&
Yohana 12 : 24

24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.

MAANDIKO YA LEO:
Kutoka 15 : 10 - 27

10 Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.

11 Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?

12 Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza.

13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.

14 Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika.

15 Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.

16 Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee Bwana, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.

17 Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana, kwa mikono yako.

18 Bwana atatawala milele na milele.

19 Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.

20 Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.

21 Miriamu akawaitikia, Mwimbieni Bwana kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.

22 Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.

23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.

24 Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?

25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko;

26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.

27 Wakafikilia Elimu, palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na mitende sabini; wakapanga hapo, karibu na maji.

HOJA ZA MAOMBI
1. TOBA
2. JIOMBEE UJASIRI WA KI- MUNGU NDANI YAKO.
3. KATAA MADHARA YA HOFU YA MABADILIKO KTK YAKO


Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro

Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053

Комментарии

Информация по комментариям в разработке