DAZ NUNDAZ-BARUA

Описание к видео DAZ NUNDAZ-BARUA

Daz Nundaz - Barua
Oya namna gani mzee, ah, mbona leo uko hivi mzee, basi tuuu.
Vipi mchizi wangu mbona naona umesizi, unaonekana kama moyoni una majozi, au dili zako leo haziendi sawa, jinsi unavyoonekana kama umepagawa, niambie ili nielewe ili na mie nisipagawe, kwani tangu nimefika nakuona umepooza, hebu niambie kitugani unachowaza, sema basi, ni nini kinachokusumbua nafsi, niambie basii au kuna kitu kimekuugasi.
Aah we mola acha tuu wangu mkachaa, ni story ndefu nikianza kukupaa, ubongo wangu nahisi kama unazafilika, kwa haya matatizo makubwa yaliyonifika, shemeji yako nadhani unamjuaa, ambaye kichwa changu alikichenguaa,
Baada ya kuishi muda mrefu na wangu lazizii, ikabidi niende kuwataarifu wazazii, kwamba nimeshampata mwenzanguuu, ambaye nitafunga naye pingu za maisha, na nilikuwa na hakika hakuna ambaye atatutenganishaa, basi bwana baada ya kurudi yangu safarii, nikakuta mlango wa gheto umepigwa kufulii, nauliza watu wote sipati jiiibu, niko zangu kwa mwenzako ulionisibuu, nikaanza kusaga tunda langu kwa sanaa, lakini jitihada mwisho zikashindikana, nikaamua basi tu mi kutulizana, nikawasitoki nje nipo ndani tu nalalaa, huku mawazo mengi kichwani yamenitawalaa,
KIITIKIO
Katika mahaba tulishazama dibwnini lakini barua niliopokea nashindwa hata kuamini, ua langu moyo wangu halipo tena na mimi,barua hii, jamani inanihuzunishaa, kila nisomapo moyo unasononekaa,na ufukara ndio uliotutenganishaaaa,
subiri basi story nikumalizie
enhe
mkasa huu mwanangu ulionifika mie
enhe
hususani imepita wiki kadhaa, ndipo hapo nikapokea baruaa, kilichokuwa ndani sikukitambuaa, nikaja kuelewa baada ya kuifunguaaa, nikakuta barua yenye ujumbe mzito, ikiwa imeambatana na kadi ya mwaliko, ndege wangu ameluka hayupo tena namii, sasa hivi sijui mwenzangu mimi nanii, hali yangu duni imenifanya kuelemewa, na hivi karibuni demu wangu anaolewa. barua inanisisitiza Harusini niuruliee, sijui siku hiyo hata wapi mi nianziee, mpenzi umeniacha kwenye nyavu nimenasa, nimebaki kama kipofu sioni pa kupapasa, nikisoma barua hii kumalizia huwa nashindwaa, kwani nahisi kama ulivyonishadundaa,
Shika mwenyewe usome barua eeh, soma mwenyewe uone barua eeh, shika mwenyewe usome barua eeh, soma mwenyewe uone barua eeh
Ikufikie wangu wa enzi mpenzi,mi kiafya mzima, natumai na we kiafya uhai,dhumuni la barua ni kukutaka na wewe kujua, mimi ni Assa na kipi kisa na mkasa, kilichonishawishi bali nawe mpenda kuishi, sio siri mimi binafsi kupenda kuishi maisha duni ya chini sana, kumbuka ufukara umasikini kututenga vimechangia, ila usipinge bwana,sasa nani alaumiwe unadhani, hivi punde tu nataraji kufunga pingu maishani ili niishi maisha ya thamani, yaliyogharama tena adimu na tena adimu kama Almasi, fanya hima usikose harusini ukipata nafasii, katika barua hii nimeambatanisha kadi hii ya mwalikoo ni yakoo.......
Basiii usimalizie kusoma, basiii usimalizie kusoma, Kwani ukiendelea moyo wangu unauchomaa kwa kuondoka wangu huyu mpenzii, moyo wangu umejawa na simanzi, niliamini tutatenganishwa na umauti, sasa nimekubali fukara hana sauti, molla ndiye anayegawa umasikini na utajirii, naye hali yangu mpenzi ameshindwa kuihimilii, na ndio maana unaniona leo nimeshika taama, utadhani kifaranga aliyekosa mama, aliyemgaia yeye ndie aliyenipa mimi ufukaraa, lakini naamini ipo siku nyota yangu itang'araa.
KIITIKIO
Katika mahaba tulishazama dibwnini lakini barua niliopokea nashindwa hata kuamini, ua langu moyo wangu halipo tena na mimi, barua eeh, jamani inanihuzunishaa, kila nisomapo moyo unasononekaa, na ufukara ndio uliotutenganishaaaa.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке