KILICHOTOKEA KABLA YA AJALI ILIYOUA WATU 12 MBEYA, YASEMEKANA DEREVA ALISHINDWA...

Описание к видео KILICHOTOKEA KABLA YA AJALI ILIYOUA WATU 12 MBEYA, YASEMEKANA DEREVA ALISHINDWA...

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa ametaja chanzo cha ajali iliyoua watu 12 na kujeruhi 23, akisema ni dereva kushindwa kuchukua tahadhari kwenye mteremko na kusababisha gari kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea jana Septemba 27, 202 baada ya gari aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likitokea Mbalizi kuelekea kwenye mnada katika kijiji cha Jojo, Kata ya Ilembo wilayani Mbeya kuacha njia na kupinduka.

Hii ni ajali ya tatu ndani ya mwezi huu, ikitanguliwa ile ya Septemba 4, iliyohusisha basi la kampuni ya Shari Line iliyoua watu tisa na kujeruhi wengine 18 huko Kata ya Chimala wilayani Mbarali na kampuni ya A-N Classic iliyoua 12 na kujeruhi 44, Septemba 6.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 28, 2024, Kamanda Siwa amesema ajali hiyo ilitokea saa 2:30 asubuhi.
"Dereva alikimbia baada ya ajali, Polisi inaendelea kumsaka wakati majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha Afya Ilembo.
“Tunatoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama na kuacha kupakia abiria kwenye magari ya mizigo," amesema Kamanda Siwa. Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Video na Johnson James

Комментарии

Информация по комментариям в разработке