Familia kadhaa zaathirika kwenye zoezi la bomoamoa mtaa wa Makasembo, Kisumu

Описание к видео Familia kadhaa zaathirika kwenye zoezi la bomoamoa mtaa wa Makasembo, Kisumu

Familia kadhaa katika mtaa wa Makasembo zimeachwa bila makao baada ya makaazi yao kubomolewa na tinga za kaunti ya Kisumu hapo jana.
Maeneo ya kuabudu ni miongoni mwa majengo yaliyobomolewa kwenye zoezi hilo ambalo limesababisha uharibifu mkubwa wa mali ya thamani isiyojulikana. Aidha wakaazi wamelalamika hatua hiyo wakisema hawakupewa ilani ya ubomozi huo unaonuia kutwaa nafasi ya ujenzi wa miundo msingi kwa matayarisho ya kongamano la miji ya Afrika litakalofanyika mwezi septemba mwaka huu. Kwa upande wake meneja  wa mji wa Kisumu alisisitiza kwamba wataendelea na ubomozi huo ili kuboresha jiji hilo kwa maandalizi ya Afri-Cities mwakani

Комментарии

Информация по комментариям в разработке