DAKIKA 90 ZA TAIFA STARS VS EQUTORIAL GUINEA

Описание к видео DAKIKA 90 ZA TAIFA STARS VS EQUTORIAL GUINEA

DK 90 ZA TAIFA STARS VS E GUINEA

LEO Novemba 15 timu ya Taifa ya Tanzania itamenyana na timu ya Taifa ya Equatorial Guinea kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kuwania kushiriki michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyika 2021.

Kwenye jumla ya mechi 4 za ushindani ambazo timu hiyo ya Taifa ya Equatorial Guinea imecheza hakuna hata mechi moja ambayo wameambulia ushindi zaidi ya kupata sare na vichapo wakiwa ugenini tofauti na Stars ambayo imeambulia ushindi ikiwa ugenini mbele ya Sudan kwa kuifunga mabao 2-1.

Ilipoteza mbele ya timu ya Taifa ya Congo kwa kufungwa bao 1-0 pia ililazimisha sare ikiwa nchini Sudan Kusini ya kufungana bao 1-1 pamoja na ule dhidi ya Chad kwa sare ya kufungana mabao 3-3, na iliambulia kichapo mbele ya Saudi Arabia kwa kufungwa mabao 3-2.

Kwenye jumla ya mechi nne ikiwa ugenini imefungwa jumla ya mabao nane huku wao wakifunga mabao sita pekee.

Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania, Juma Mgunda amesema kuwa wanatambua ugumu wa mchezo watapambana kupata matokeo.

“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu tutapambana kupata matokeo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.


YALIYOMO GLOBAL TV ONLINE (+255 657 955825 au +255 784 888982)
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
HABARI MPYA DAILY:
https://www.youtube.com/playlist?list...

HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA:
https://www.youtube.com/playlist?list...

GLOBAL RADIO TV:
https://www.youtube.com/playlist?list...

EXCLUSIVE INTERVIEW:
https://www.youtube.com/playlist?li

Комментарии

Информация по комментариям в разработке