Waefeso 1:3 *Atukuzwe Mungu*, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
6 Na *usifiwe utukufu wa neema yake*, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
8 Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;
11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.
13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; *tena mmekwisha kumwamini yeye*, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
_____
[Intro]
Lead: Utukuzwe Mungu…
Utukuzwe Mungu;
Baba wa Bwana wangu, Yesu Kristo oo oh…
[Verse 1]
Lead: Uliyenibariki
kwa baraka zote;
ndani yake Kristo,
Choir: Ndani ya Kristo
Lead: Ulinichagua,
ili niwe mtakatifu,
nisiye na hatia
mbele zako.
Choir; Bwana,
mbele zako…
[Chorus]
Choir: Usifiwe utukufu wa neema yako!
Lead: wa Neema yakooo,
Choir: wa neema yakooo!
Lead: Ambayo
Choir: umenineemesha katika Kristo.
Lead: Katika Kristoo ooh…
All (together):
Usifiwe!
Usifiwe!
Ee Mungu
u mwema!
[Verse 2]
Lead: Katika Yesu,
kwa damu yako,
nina ukombozi wangu.
Choir (echo): Ukombozi wangu!
Lead: Msamaha wa dhambi,
sawasawa na wingi
wa neema yako,
Neema yako…
Choir: neema yako!
Lead: Ndani yako Kristo, Choir: umeniweka mrithi.
Choir: Umeniweka mrithi.
Lead; Katika Yesu,
niwe sifa ya utukufu wako!
Choir: sifa ya utukufu WAKE
Lead: Nimeweka tumaini langu,
ndani yako Kristo.
Choir: Tumaini langu,
ndani yako Kristo!
[Chorus:
Lead: Ohh...
ALL: usifiwe utukufu wa neema yako!
LEAD: wa Neema yako,
Choir: wa neema yako!
Lead: Ambayo,
ALL: umenineemesha,
katika Kristo!
LEAD: Katika Kristo oo ooh!
OUTRO
Lead: Umenitia mhuri,
kwa Roho wako Mtakatifu!
Choir:
Roho Mtakatifu!
Roho Mtakatifu!
Lead: Wewe ndiye tumaini languuu!
Choir : Tumaini langu,
Haleluya!
Lead : halelaluya
Choir: halelaluya
Lead: Wewe ndiye tumaini langu!
Choir: Utukuzwe Mungu…
Lead: Utukuzwe Mungu…
Choir: Utukuzwe Mungu…
ALl: Baba wa Bwana wangu Yesu Kristo…
Choir (echo): Yesu Kristo…
Lead; (fade with worship): Haleluya…
Haleluya…
Информация по комментариям в разработке