Mahafali ya pili shahada ya Sayansi ya kijeshi, IAA na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (Monduli)

Описание к видео Mahafali ya pili shahada ya Sayansi ya kijeshi, IAA na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (Monduli)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatunuku wanafunzi 61 shahada ya Sayansi ya Kijeshi kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa ushirikiano na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA), 22 Nov 2021.

Sherehe hizo za mahafali ya pili ya mafunzo ya kijeshi zimefanyika katika viwanja vya chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.

Mahafali haya yalienda sambamba na Kutunukiwa Kamisheni maafisa wanafunzi 118 ambapo 61 ni wa shahada ya sayansi ya kijeshi (Bachelor Degree in Military Science) na 56 wamehitimu katika Jeshi la Anga, ambapo kwa ujumla wanaume walikuwa 99 na wanawake 19.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке