LINDA IMANI (OFFICIAL VIDEO) - St. Benedict Catholic Choir - Rapogi

Описание к видео LINDA IMANI (OFFICIAL VIDEO) - St. Benedict Catholic Choir - Rapogi

Performers: St. Benedict Catholic Choir - Rapogi
Producer: Verony Productions Ltd.
Copyright ©Verony Productions Ltd.

COMPOSER: Ochieng' Odongo

Linda imani yako, linda {tunasema},
Ndugu linda imani yako, linda siku zote
Tetea imani yako, tetea {tunasema},
Ndugu tetea imani yako, tetea siku zote {hakika} *2

Tunaishi kwa neema tu,
Tunaishi kwa neema tu
Tunaishi kwa neema tu {kweli}
Neema yake Mungu * 2

Watu wengi hutafuta msaada kwa waganga,
Kila siku wao kweli wanajiita wakristo,
Hawajui kwamba Mungu ndiye, anaweza yote.

Hudhuria jumuiya na ibada mbalimbali,
Jumuiya sio eti kina mama pekee yao,
Hata sisi kina baba wote tukashirikishwe.

Kila siku yakupasa ndugu usali rosari,
Nazo sala za kanisa usije ukasahau,
Amri zote zake Mungu Baba na ukazitii.

Yastahili ubatizwe upewe kipaimara,
Ekaristi mwili na damu ya Yesu,
Utashiba, utaburudika maishani mwako.

Mkitaka kuoana, basi mkafunge ndoa,
Ili Mungu abariki maisha yenu ya ndoa,
Na watoto wenu mwakuze kwa maadili mema.

Na kwa wale wenye wito wa kushiriki ndoa,
Wanapewa sakramenti ile ya upadrisho,
Ili wao watuhudumie katika imani.

Na wakristu kati yetu wanapokuwa wagonjwa,
Wakapewe sakramenti ya upako wa wagonjwa,
Kwa imani watapata nguvu na matumaini.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке