FURAHA NA NYIMBO -FAUZIA

Описание к видео FURAHA NA NYIMBO -FAUZIA

#Taarabasiliazanzibar #oldisgoldzanzibar #taarab
Furaha na nyimbo , mpenzi kaniahidi
Pendo la urembo , kito chake zumaridi
Kupendwa ni pambo, ni ureda na maidi
Na sasa sijambo , sijambo tena Zaidi

Furaha!furaha!, kaitikia mpenzi
Kaja kwa madaha, kaja mikono iwazi

Alinisumbua , nikadhani mkaidi
Mara katua, mpenzi kapiga hodi
Kaja na maua , kaniletea zawadi
Mapenzi halawa, kila raha nafaidi

Aliniadhibu , kama kupigwa na radi
Mara kanijibu, ile labeka ya sudi
Kaniita muhibu, akafungua fuadi
Dhiki zikaghibu , na hali yangu shadidi

Akitabasamu , yamoto huwa baridi
Mpenzi mtamu , kila chake maridadi
Ni ladha adimu , raha ilozidi hadi
Msinilaumu , kila raha nafaidi

Комментарии

Информация по комментариям в разработке