MY LEGACY ILIVYOJIPANGA KUJENGA UWEZO KWA WANAWAKE, WALEMAVU na VIJANA KUMILIKI ARDHI...

Описание к видео MY LEGACY ILIVYOJIPANGA KUJENGA UWEZO KWA WANAWAKE, WALEMAVU na VIJANA KUMILIKI ARDHI...

MY LEGACY ILIVYOJIPANGA KUJENGA UWEZO KWA WANAWAKE, WALEMAVU na VIJANA KUMILIKI ARDHI...

Taasisi ya MY LEGACY imejipanga kufanya uchechemuzi wa kubadili fikra na mitizamo lakini pia kuwajengea uwezo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kuwa na uelewa na taarifa sahihi za umiliki ardhi.

Pia imejipanga kutoa ushawishi kwa makundi hayo matatu kushirikishwa katika utoaji maamuzi kwenye ngazi zote za familia, mabaraza ya ardhi n.k
Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MyLEGACY Fortunata Temu wakati akizungumza katika mkutano wa wadau, uliokuwa na adhma ya kujadili namna ya kufanya uchechemuzi wa haki za wanawake, vijana na watu wenye ulemavu za kujipatia makazi bora lakini pia ardhi na Haki za umiliki wa mali.

"Sisi kama MyLEGACY tunatekeleza mradi ambao unalenga katika kuboresha mazingira ya kujifunzia pamoja na mazingira ya kuishi na katika kufanya hilo tumeona ni lazima tuelewe Hali halisi ya makundi haya ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu."

"Bado uhitaji wa Elimu upo kwenye jamii hivyo wadau waendelee kuhakikisha wanafanya uchechemuzi na kushirikisha jamii kuhusu haki ya umiliki wa ardhi na kujua wapi wanaweza kwenda kudai haki zao."


============================================================
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 713 750910), ( +255 783453136)
⚫️ Email: [email protected]

⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI:    • Habari zote za michezo na Burudani Ta...  
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua
⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Комментарии

Информация по комментариям в разработке