Makonda Atinga Kwa Wamasai Ngorongoro "SITASHIRIKI KUGANDAMIZA HAKI ZA WATU, NITAPIGA NYUNDO"

Описание к видео Makonda Atinga Kwa Wamasai Ngorongoro "SITASHIRIKI KUGANDAMIZA HAKI ZA WATU, NITAPIGA NYUNDO"

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesisitiza kuwa hatashiriki kukandamiza haki ya mtu mahala popote pale atakapokuwa, huku akikumbusha kuwa nafasi wanazopata viongozi ni upendeleo wa Mungu.

Makonda ameyasema hayo leo Ijumaa Agosti 23, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi kutoka kata 11 zilizopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha katika eneo Oloirobi, Kata ya Ngorongoro ambapo ameambatana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, William Lukuvi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке