NIMEKUTUMAINI WEWE BWANA - KWAYA YA FAMILIA TAKATIFU

Описание к видео NIMEKUTUMAINI WEWE BWANA - KWAYA YA FAMILIA TAKATIFU

Tumsifu Yesu Kristu,
Tunaendelea kuwakaribisha kujipatia album yetu mpya ya video inayoitwa HERI KUCHAGUA JINA JEMA. Wimbo huu unaoitwa NIMEKUTUMAINI WEWE BWANA na kuimbwa na KWAYA YA FAMILIA TAKATIFU KUTOKA KANISA KUU LA MTAKATIFU YOSEFU JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM (SAINT JOSEPH'S CATHEDRAL) ni utunzi wake marehemu JOSEPH MAKOYE ambaye ni mmoja kati ya watunzi mahiri sana katika nyanja hizi za mziki Mtakatifu Tanzania, baadhi ya nyimbo zingine alizotunga ni kama Hiki ni chakula na Subira ya Mkulima.

Album hii imesheheni nyimbo kemkem ambazo ni

1. Mfanyieni Bwana Shangwe - P.F Mwarabu
2. Aliyeacha nyumba - Celestine Kapama
3. Aleluya Mshukuruni Bwana - Charles Saasita
4. Gloria - Antonio Vivald
5. Heri kuchagua jina jema - Richard Mloka
6. Ave Maria - Bach/Gounod
7. Tufuate Mfano - Fortunatus B. Mallya
8. Miaka 150 ya Ukristo Tanzania - David Benjamin Wasonga
9. Mwimbieni Bwana - Celestine Kapama
10. Nimekutumaini - Joseph Makoye
Kwa mahitaji ya album hii wasiliana nasi kwa simu namba +255755816669/0659557769


MANENO YA WIMBO (MUSIC LYRICS)
NIMEKUTUMAINI – J. MAKOYE
Nimekutumaini wewe e Bwana, nimekutumaini wewe ee Bwana
Nimesema wewe u Mungu wangu, siku zangu zimo mikononi mwako
1. Nimekukimbilia wewe ee Bwana
Nisiaibike milele, kwa haki yako yako uniponye
2. Wewe ndiwe genge langu na ngome yangu
kwa ajili ya jina lako, uniongoze unichunge
3. Wewe ni nuru yangu unimulike
wewe ndiwe wokovu wangu, uniokoe na adui

Комментарии

Информация по комментариям в разработке