ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA NA WENZAKE 6 WAACHIWA HURU "HALI YANGU SIO NZURI"

Описание к видео ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA NA WENZAKE 6 WAACHIWA HURU "HALI YANGU SIO NZURI"

Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imewaachia huru washitakiwa saba akiwemo aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia tiketi ya Chadema Jimbo la Bukoba Mjini 2020 Chief Kalumuna ambao walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa nane yakiwemo ya kusababisha fujo,kutotii,kusababisha uharibifu wa mali siku ya kuwaapisha mawakala na wagombea tarehe 21 mwezi wa 10 mwaka 2020

Hakimu Mkazi wa Mahaka ya Bukoba Joseph Lwambano amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuthibitishwa hivyo inaonyesha washitakiwa hawakuhusika

Akiongea nje ya mahakama mshitakiwa namba moja Chief Kalumuna ameeleza furaha yake baada ya kuachiwa huru

Комментарии

Информация по комментариям в разработке