MRADI HUU UMETUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA NA UPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA MAJARIBIO

Описание к видео MRADI HUU UMETUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA NA UPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA MAJARIBIO

Meneja TEMESA   Kikosi cha Umeme, Mhandisi Pongeza Semakuwa amesema mradi wa usimikaji wa taa za barabarani kwa Barabara za mabasi yaendayo haraka/mwendokasi (BRT phase II) baina ya TEMESA na kampuni ya SINO HYDRO kutoka nchini China umewapa ujuzi na kuwajengea uzoefu mafundi wa TEMESA.

Mhandisi Pongeza ameyasema hayo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo eneo la makutano ya Barabara ya Chang’ombe na Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba ambapo TEMESA imeshiriki kusimika taa za barabarani kwenye Barabara za mabasi yaendayo haraka/ mwendokasi 53.

Mhandisi Pongeza amesema ufungaji wa taa hizo upo katika hatua za mwisho za majaribio na makutano yote 53 yameshakamilika pamoja na ufanywaji wa majaribio ya awali ambapo pia amesema mafundi 5 wamejipatia uwezo wa namna ya kuzihudumia taa hizo.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке