Tafakari Dominika ya 20 ya Mwaka A wa Kanisa: Ukatoliki wa Imani na wa Kanisa

Описание к видео Tafakari Dominika ya 20 ya Mwaka A wa Kanisa: Ukatoliki wa Imani na wa Kanisa

Masomo Dominika 20 Mwaka A yanatualika tutafakari juu ya “ukatoliki” wa Kanisa. Neno katoliki linamaanisha kitu kilichoenea pote, kitu kilichokamilika na tena kinachowajumuisha wote. Kanisa, kama sakramenti ya wokovu, ni katoliki: limeenea pote ili kuwafikia wote, limekamilika kwa maana ya kuwa na uwezo wa kutenda kadiri ya asili yake na linawajumuisha wote bila ubaguzi wa aina yoyote na kuweka mbele yao wokovu ili kila mmoja aweze kuupokea kwa imani.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке