MALI ZA BILIONEA MSUYA ZAANZA KURUDISHWA KWA WATOTO NA SERIKALI

Описание к видео MALI ZA BILIONEA MSUYA ZAANZA KURUDISHWA KWA WATOTO NA SERIKALI

WATOTO WA BILIONEA MSUYA WARUDISHIWA NYUMBA NA SERIKALI

Arusha. Mgogoro wa mali za billionea Erasto Msuya Serikali yaagiza watoto wa kurejeshwa kwenye makazi ya Baba yao ambayo ulikuwa imefugwa.

Agizo hilo la awali ametolewa Leo Octoba 17, Mkuu wa wilaya ya Arumeru,baada ya kukutana na wazazi wa billionea Msuya, watoto wake na baadhi ya wanafamilia upande wa mke wa Msuya ambaye yupo magereza segerea akikabiliwa na kesi ya mauji.

Mke huyo wa billionea Msuya anatuhumiwa kwa mauaji ya dada wa billionea huyo, Aneth Msuya yaliyotokea Kigamboni jiji Dar es salaam.

Wakizungumza baada ya maamuzi hayo,Mtoto wa billionea huyo,Kelvin Msuya na Baba wa billionea huyo,Elisaria Msuya walikubaliana na maamuzi hayo ya awali.

Kelvin (22)anasema, anataka yeye na wadogo zake wapewe haki ya kusimamia Mali za Baba na mama yao na sio mtu mwingine.

Anasema familia ya baba yao inataka kuwanyan'ganya mali kwani baada ya mama yao kukamatwa wamefungua kesi upya za kudai usimamizi wa mirathi ingawa tayari mama yetu aliteuliwa wa lengo lao wachukuwe Mali.

"Mwanzo babu na shangazi Ester walifungua kesi ikafutwa, Ndeshukuro Sikawa na babu wakafungua ikafutwa sasa amefunguatena Bibi peke yake"amesema

Anasema ndugu hao walinfungulia kesi na kutaka kumuunganisha na mama yake lakini alisaidiwa na ndugu wa mama yake na maafisa wa juu wa polisi

Hata hivyo baba wa billionea huyo, anasema walifunga nyumba za billionea huyo,kutokana na kuzuia upotevu wa Mali hasa baada ya kuanza kuibiwa

Hata hivyo alisisitiza baadhi ya Mali za billionea huyo yeye na mkewe walikuwa na hisa ikiwepo mgodi wa Tanzanite ambao alidai ni mali yake,hoteli ya SG na mashamba.

Billionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka Agost 7 2013 na ameacha nyumba za kifahari zaidi ya tano,magari,hoteli mbili za kitalii,viwanja na mgodi wa Tanzanite.
HABARI MPYA DAILY
https://www.youtube.com/upload?redire...
https://www.youtube.com/playlist?list...

HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA:
https://www.youtube.com/playlist?list...

GLOBAL RADIO TV:
https://www.youtube.com/playlist?list...

EXCLUSIVE INTERVIEWS:
   / playlist  

Комментарии

Информация по комментариям в разработке