Utacheka Utani Wa AY Kwa Fid Q "Fid q Ni Shabiki Yangu, Siku Hizi Ana-smile" | Salama Na AY PART 2

Описание к видео Utacheka Utani Wa AY Kwa Fid Q "Fid q Ni Shabiki Yangu, Siku Hizi Ana-smile" | Salama Na AY PART 2

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

THE ARCHITECT

Sasa ule usemi wa ukitaka kujua tabia za mtu waangalie Rafiki zake pengine unaweza kuanzia hapa kwa mtu ambaye atakua anataka kunifahamu mimi vizuri, maana hakuna mtu ambaye hajui ukaribu uliopo kati yangu na Ambwene Yessayah, kabla hatujakua na vitambi na kutambulika kwa majina yetu mawili sisi tayari ni marafiki, na pengine sasa tumeshakua ndugu.

Yeye kazaliwa Mtwara huko nami nimezaliwa Unguja, wazazi wake ni kama wazazi walonilea mimi, mara nyingi kulikua na transfer za kazi kwao kwahiyo kuhama kutoka mkoa mmoja na kwenda mwengine kila baada ya miaka kadhaa ilikua jambo la kawaida tu, ingawa lilikua linakera haswa kwa kina Kaka na Dada zetu ambao tayari wao walishakua wakubwa kiasi na washajichagulia marafiki zao, ilikua tafrani tena kuanza kutafuta marafiki wapya na kuhamia shule mpya na mazingira mapya kabisa. Ila hili ndo pengine limemfanya Rafiki yangu Ambwene Allen Yessayah awe mbunifu na muerevu katika maisha yake na kazi zake ambazo amekua akizofanya kwa umahiri kwa zaidi ya miaka 18 sasa.

Miaka ya karibuni AY atatimiza miaka 40 toka amekuja hapa duniani na kwa bahati mbaya wazazi ambao wamemleta duniani walishatangulia mbele ya Haki na Mwenyezi Mungu Awarehemu, ila AY anakumbuka mahusiano yake na Mzee wake, wakati anakua, ukaribu wao, kazi ambazo alikua anazifanya na pia alikua Baba wa aina gani. Mahusiano yake na Kaka yake na Dada zake wawili (Dada mmoja mkubwa na mwengine mdogo wake wa mwisho) ni ya karibu sana. Yeye alichukua jukumu la kuwa ‘Baba’ mara baada ya kuanza kutengeneza pesa kwenye fani yake na mpaka Marehemu Mama yake anatangulia mbele ya haki alikua anakaa kwenye nyumba ambayo Ambwene alikua anaiangalia.

So nini kilimfanya achague muziki? Mama yake alikua radhi na hili? Kuhusu shule je ambayo alikua yuko vizuri nayo tu? Aliachana nayo vipi? Mahusiano yake na East Coast Team? Mwana FA? Muziki na pesa? Yeye kuwa wa kwanza kurekodi na kufanya shows nje ya Tanzania? Vipi kuhusu industry hii na maendeleo yake? Je tuko sehemu salama? Sehemu nzuri? Future yeye hasa anaionaje?

Kuna mengi yalifaa kuongelewa humu ila kuna na mengine ambayo wakati wake wa kuyazungumza haukua muafaka, lakini suala la yeye kuwa Baba kwa mara ya kwanza hatukuweza kuliacha liende bila ya sisi kutoa hongera zetu. Aviel ndo jina la kijana wake wa kwanza, experience ya kupata mtoto kwa mara ya kwanza nayo hatukuiacha kuizungumzia.

Yangu matumaini kama ilivyo ada, utayaelewa maongezi yetu haya na kutakua na mawili matatu ya kujifunza ndani yake.
Nakutakia uangaliaji/usikilizaje mwema.

Love,
Salama.




Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Комментарии

Информация по комментариям в разработке