KIBOKO YA WACHAWI AWATUKANA WATANZANIA AWAITA WAPUMBAFU | AFUNGUA KANIS...

Описание к видео KIBOKO YA WACHAWI AWATUKANA WATANZANIA AWAITA WAPUMBAFU | AFUNGUA KANIS...

Ibada ya kwanza ya Nabii Kiboko Ya Wachawi iliyohudhuliwa na mamia ya watu nchini Congo, Lubumbashi wiki chache baada ya kusimamishwa kuendelea na huduma pamoja na kufukuzwa nchini Tanzania..
Hii inatia faraja na matumaini kwake na kwetu pia ambao tulitamani kuona akiendelea na huduma yake ya kuua wachawi na kuangalia chupi za washirika wake huko huko kwao. Nitoe angalizo kwa watumishi wa Mungu nchini Tanzania haswa wazawa mnaomtumikia Mungu hapa nyimbani. Fanyeni huduma zenu kwa kuheshimu sheria za nchi na pia kuzingatia desturi na maadili kama tulivyopokea injili kutoka kwa wazee wetu. Hawa wageni haswa wanaoleta injili ngeni siyo wa kuwaiga kabisa maana yakiwakuta ya kuwakuta wana nyumbani kwao pa kukimbilia, ila mimi na wewe hatuna sehemu nyingine ya kukimbilia. Hivyo basi tujitahidi kuilinda hadhi ya injili na heshima ya utu sawasawa desturi yetu ya kitanzania pasipo kubebwa na mkumbo wa mgeni yeyote ambaye atashindwa kuheshimu mambo hayo ya msingi. Nimalizie kwa kuitaka familia ya Kiboko Ya Wachawi ikiwa ni mke, watoto, washirika na watenda kazi kuanza safari ya kwenda Lubumbashi ili wakaendeleze moto ule wa buza huko huko kwao. Hapa Tanzania watabakia wale wenye sura na tabia ya Kristo ambayo ilitambulishwa na wazee wetu wenye maadili kama vile Moses Kulola na wengineo.
Waliobakia woote ambao wameiga mfumo mbaya wa injili ngeni na wao waanze kutafuta ukumbi wa kuanzisha huduma huko Lubumbashi maana siku zao zinahesabika...

Комментарии

Информация по комментариям в разработке