Deusdedith Soka: Haijalishi Watatutesa Kiasi Gani ni Lazima Tuipiganie Nchi Yetu

Описание к видео Deusdedith Soka: Haijalishi Watatutesa Kiasi Gani ni Lazima Tuipiganie Nchi Yetu

Mwanaharakati, Deusdedith Soka, siku kadhaa kabla ya kuripotiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana alifanya mahojiano na The Chanzo na kusema kuwa amekuwa akikumbana na vitisho mbalimbali vya kutaka kumdhuru ili kuirudisha nyuma nia yake ya kupambania demokrasia nchini lakini suala hilo halitamrudisha nyuma kamwe.

Soka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) wilaya ya Temeke, aliyasema hayo Agosti 16, 2024, wakati alipozungumza nasi kwenye mahojiano maalum.

Mazungumzo hayo pia yaligusia mpango wake wa kuandaa maandamano yaliyopangwa kufanyika Agosti 26, 2024, kwa ajili ya kuishinikiza Serikali ichukue hatua kukomesha matukio ya utekaji pamoja na kurejesha mchakato wa kuipatia Tanzania Katiba Mpya.


Unaweza kutufuatilia kupitia;

TWITTER:   / thechanzo  
INSTAGRAM:   / thechanzo  
FACEBOOK:   / thechanzo  
TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com

Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105

The Chanzo Initiative, 2024 © All Rights Reserved.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке