WAZIRI ABANANISHWA BUNGENI UMRI WA KUAJIRIWA, SPIKA ARUHUSU MJADALA, WABUNGE WACHACHAMAA

Описание к видео WAZIRI ABANANISHWA BUNGENI UMRI WA KUAJIRIWA, SPIKA ARUHUSU MJADALA, WABUNGE WACHACHAMAA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa ya mwaka 2024 amesema katika marekebisho hayo kifungu cha 25 kinapendekeza kuwepo kwa masharti ya ziada ya kupambana na rushwa ya ngono.

Katika masharti hayo yanalenga kutoa adhabu kwa mtu anayeomba rushwa ya ngono kwa kutumia ushawishi wa mamlaka aliyonayo na mtu anayeshawishi au anayetoa ahadi au kutoa

“kifungu cha 25 kwasasa kinatoa adhabu kwa mtu aliye kwenye nafasi ya madaraka anayedai rushwa ya ngono bila kumwajibisha anayemshawishi aliye katika nafasi ya madaraka kutenda rushwa ya ngono kifungu hiki yanamlenga mtu anayeomba rushwa ya ngono kwa kutumia ushawishi kwa mamlaka aliyonayo na mtu anayeshawishi au anayetoa ahadi au kutoa rushwa kwa mtu aliye na madaraka” George Simbachawene

Комментарии

Информация по комментариям в разработке