Mwokozi Wetu Anatupa Furaha Nyimbo za Wokovu 141 Tabernacle Chrétien de Lubumbashi

Описание к видео Mwokozi Wetu Anatupa Furaha Nyimbo za Wokovu 141 Tabernacle Chrétien de Lubumbashi

Mwokozi Wetu Anatupa Furaha Nyimbo za Wokovu 141 Tabernacle Chrétien de Lubumbashi

1.
Mwokozi wetu anatupa Furaha duniani,
Atuongoza kwa neema Na anatushibisha.
Tazama, Yupo pamoja nasi, Neema haitaisha kamwe !
Haleluya, Haleluya, Haleluya, Amina !

2.
Ni vema kumpenda Mungu Aliyetukomboa,
Vizuri kuwa mtu Wake, Sitapotea kamwe.
Furaha yetu itabakia, Ikiwa vyote vingetoweka.
Haleluya, Haleluya, Haleluya, Amina !

3.
Ikiwa giza mara nyingi, Na jua likifichwa,
Na tukijaribiwa huku, Twajuwa ni kwa muda.
Mbinguni hatutaona kamwe huzuni wala machozi tena.
Haleluya, Haleluya, Haleluya, Amina !

4.
Na tusisumbukie tena Chakula wala nyumba,
Maana vyote twavipata Kwa ne’ma yake Mungu.
Njiani yote atuongoza, Aichukuwa mizigo yetu.
Haleluya, Haleluya, Haleluya, Amina !

5.
Ikiwa vema huku chini Kutegemea Yesu,
Furaha gani huko juu Kuona uso wake !
Tutaiona furaha tele, Na utukufu hautaisha,
Haleluya, Haleluya, Haleluya, Amina !

Below is the link to the video where the song was extracted:
   • Dimanche 16-06-2024 ''LES SAGES COMPR...  

Mwokozi Wetu Anatupa Furaha Nyimbo za Wokovu 141 Tabernacle Chrétien de Lubumbashi

#Maranatha

Комментарии

Информация по комментариям в разработке