USALAMA WA RAIA WETU NI SWALA LA LAZIMA

Описание к видео USALAMA WA RAIA WETU NI SWALA LA LAZIMA

KLINIKI MAALUM YA DC ARUSHA KUANZA KESHO, KUTEKELEZA AGIZO LA RC MAKONDA.


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa anatarajia kuanza Kliniki maalum ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto Mbalimbali za wananchi wa Wilaya ya Arusha kuanzia kesho jumatano Mei 22-24 Ofisini kwake Jijini Arusha.

Akizungumza na Wanahabari ofisini kwake leo Mei 21, 2024, Mhe Mtahengerwa amesema kliniki hiyo inafanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda alilolitoa Mei 10,2024 wakati wa hitimisho la kliniki yake ya Mkoa.

Mhe. Mtahengerwa amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye Kliniki hiyo na kusema kuwa Kliniki hiyo itaanza saa mbili asubuhi ambapo kila mwananchi atapata nafasi ya kusikilizwa na kutatuliwa changamoto walizonazo.

Mhe. Mkuu wa wilaya amesema wamejinga kikamilifu kusikiliza wananchi ambapo pia kutakuwa na misaada mbalimbali ikiwemo msaada wa kisheria kwa wananchi watakaokuwa na mashauri mbalimbali kwenye mahakama za ngazi mbalimbali mkoani Arusha.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке