KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 12 AUG 2025
UJUMBE WA LEO: KUKOMESHWA KWA MAMBO YANAYO TUKWAMISHA KUPITIA KWENYE NASABA ZA UKOO KATIKA VIZAZI VILIVYOPITA ILI KUPATA UPENYO KWA VIZAZI VILIVYOPO
Kumbukumbu 32 : 8
Ayubu 8 : 8 - 10
1 Mambo ya nyakati 5 : 1
Kutoka 20 : 2 - 6
Kumbukumbu 32 - 7
1 Petro 1 : 18 - 19
Waebrania 12 : 15
Ezekieli 16 : 44 - 45
Nahumu 1 : 9
⏺️AWEPO MTU AU WATU WATAKAO SAIDIANA KUCHUKUA HATUA ZA MAKUSUDI ZA KUCHORA RAMANI YA KIROHO KULINGANA NA NASABA YA UKOO HUSIKA AU YALE MAENEO YANAYO WAHUSU
(SPIRITUAL MAPPING AND RESEARCH)
Kumbukumbu 32 : 8
8 Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
Ayubu 8 : 8 - 10
8 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;
9 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)
10 Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?
1 Mambo ya nyakati 5 : 1
1 Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza.
Kutoka 20 : 2 - 6
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kumbukumbu 32 - 7
7 Kumbuka siku za kale, Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonyesha; Wazee wako, nao watakuambia.
1 Petro 1 : 18 - 19
18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Waebrania 12 : 15
15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Ezekieli 16 : 44 - 45
44 Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake.
45 Wewe u binti ya mama yako, amchukiaye mume wake na watoto wake; nawe u umbu la maumbu yako, waliowachukia waume zao na watoto wao; mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako Mwamori.
Nahumu 1 : 9
9 Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.
Mhubiri: Mwl: Renald Mlawi
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]
Информация по комментариям в разработке