NAMTAKA MTOTO WANGU AKIWA HAI, NILIKATAA ASIENDE , KAULI YA BABA WA ANAYEDAIWA KUPOTEA MSITUNI

Описание к видео NAMTAKA MTOTO WANGU AKIWA HAI, NILIKATAA ASIENDE , KAULI YA BABA WA ANAYEDAIWA KUPOTEA MSITUNI

Arusha. "Anayehitajika kuwajibika ni uongozi wa shule, wao ni wazembe. Ninamtaka mtoto wangu akiwa hai, siyo kwamba tunashindwa kukaa naye nyumbani, tumewaletea watoto wetu muwatunze, hatudaiwi chochote. "Halafu unaniambia mnampeleka safari haonekani, hapana haiwezekani, hata jana (Septemba 16) mbele ya Ofisa wa Upelelezi nimewaambia nahitaji mtoto wangu akiwa hai, kama hawana ulinzi, ni nini walienda kujifunza huko mlimani?" Ni kauli ya Johannes Mariki, mzazi wa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bagara, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara, Joel Johannes (14) anayedaiwa kupotea tangu Septemba 14, 2024 katika Mlima Kwaraa walikokwenda kwa ziara ya masomo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Simon Mdee amesema katika safari hiyo wanafunzi 103 walienda mlimani wakiwa na walimu wao na waongozaji wapanda mlima. Amesema baada ya kushuka na kubainika kuwa Joel hayupo waongoza wapanda mlima walirudi mlimani kumtafuta hadi saa sita usiku bila mafaniko. Amesema jitihada mbalimbali zinaendelea zikiongozwa na Jeshi la Polisi, halmashauri na kushirikisha jamii ya watu wanaoishi pembezoni mwa mlima huo. Mdee amesema imeundwa timu, akiwamo Ofisa Elimu Sekondari, ambayo imeenda shuleni kuzungumza na marafiki wa Joel kupata taarifa zaidi. "Pia tumeagiza Jeshi la Akiba linaenda kuungana na waliopo kufanya operesheni ya kumtafuta," amesema.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке