Safari Ya Dina : Asimulia Msoto Aliopitia Kabla Kuwa Mtangazaji | SALAMA NA DINA MARIOUS PART 1

Описание к видео Safari Ya Dina : Asimulia Msoto Aliopitia Kabla Kuwa Mtangazaji | SALAMA NA DINA MARIOUS PART 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

Dina Marious ni STAR ambaye amakua akijenga jina lake kwa miaka mingi sana. Kama sote tunavyofahamu hakuna mtu ambaye anaibuka tu siku moja na kupata heshima na kuaminiwa kama hajafanya kazi ambayo itamfanya watu wamuamini na kumpenda. Dina yeye ameteka kabisa soko la Wanawake, kitu chochote kinachohusiana na wanawake na madhila, raha na mambo yao ya kijamii basi ukiangalia kushoto na kulia lazima utamkuta Dina yuko hapo akitoa mchango wake kwenye suala hilo. Iwe kuanzia maandalizi au uwepo wake tu. Hicho ndo ambacho yeye kama Mama na Dada na Binti ameamua kufanya, na anaweza haswa.

Alianzia Radio ya watu ya Clouds FM na baada ya kupata mtoto wake wa kwanza mitihani mingi aliipitia, ile maternity leave ambayo alikaa wakati anamkuza kijana wake ilileta mabadiliko makubwa kwenye maisha yake. Zion (mtoto wake) alipo zaliwa ilimbidi Dina aache kazi kwenye Taasisi ambayo alikua ameizoe mno na kutafuta ustaarabu mwengine bila ya kuwa na mipango hiyo wakati alipochukua likizo yake ya kwenda kujifungua. Mipango ilikua akitoka kwenye likizo yake hiyo ya uzazi basi arudi tu kazini kwake kama kawaida lakini Bosi wake wa wakati huo, Marehemu Ruge Mutahaba alikua na mipango mengine na Dina mipango ambayo kwa mujibu wake anaamini alikua akipigwa chenga tu na hakukua na mpango thabiti ambao ulikua umeekwa kwaajili yake.

Dina anakumbuka nenda rudi alizokua akizipata na kulipwa mshahara bila ya kufanya kazi yoyote, kwa kweli hilo lilikua likimsubua sana na anasema kila akiangalia kushoto na kulia alikua haoni dalili zozote za yeye kuanza kufanya kazi muda wowote wa karibu na kwasababu maswali yake mengi mazito yalikua yakipatiwa majibu mepesi mepesi aliona basi si vibaya kama atatafuta challenge nyengine kwenye maisha yake. Kwanza hiyo plan ambayo alikua amepewa hakua ameifurahia na pili majibu ambayo alikua anapatiwa nayo yalimfanya ajue pale hapakua sehemu sahihi kwake tena.

Kumuuma ilikua ikimuuma sana kama anavyosema mwenyewe, hakukua na sababu yoyote ya kutaka kufanya mabadiliko yale ambayo yalifanyika, ya kutaka kumpeleka yeye kwenye TV wakati tayari alikua ameshatengeneza kundi kubwa la mashabiki kwa wakati huo, na pengine approach iliyotumika pia haikua sahihi na hilo liliacha ladha mbaya kwenye moyo na kinywa chake, na baada ya hapo kwasababu kulikua na ofa nyengine hakufanya ajizi kuziskiliza na uzuri zaidi kwanza hapakua mbali na ofisi yake ya zamani hapo alipokua anatakiwa na pili ambalo ndo KUBWA kabisa, alikua anapewa muda ule ule wa hewani kama ambao alinyang’anywa baada ya kuenda likizo ya uzazi kwenye ajira yake ya zamani. Alikua na kila sababu ya kuchukua hatua nyengine na kujisogeza mbele zaidi, kama ambavyo tunafahamu, mtu huenda aitwapo. Na mengine ndo haya, yamebaki story tu.

Nafasi yake kwenye jumuia za wanawake ni ya kipekee na anaiweza kuikaimu vizuri tu, amekua akifanya shughuli mbali mbali za kutatua baadhi ya adha na pia kuwatunza wale ambao anadhani wanastahili ili kuwafanya wapate nguvu zaidi ya kuendelea kufanya wanayofanya kwa uzuri zaidi. Na amekua mfano mzuri hata kazini kwake maana kipindi chake cha Radio ni moja ya vipindi vinavyo sikilizwa zaidi kwa wakati ule. Hilo halina ubishi.
Kama binadamu wengine na yeye nae ana ushindi mwingi na kushindwa kwingi kwenye maisha yake na kwenye session hii tukiyagusia hayo na zaidi. Kuhusu mapenzi, mtoto, familia yake alitokea, elimu na malezi lakini pia muajiri wake wa zamani na jinsi ya kukabiliana na mambo mbali mbali maishani.

Yangu matumaini uta enjoy na kujifunza mambo kadhaa kuhusu kazi na jinsi na kujua kutafuta na kupata kutoka sehemu nyengine ukiachana na ile ulokua umeizoea.

Love,
Salama.

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Комментарии

Информация по комментариям в разработке