Jinsi ya kusali Rozari ya Mt. Mikaeli | Valeriana Mayagaya (MwanaSayuni)

Описание к видео Jinsi ya kusali Rozari ya Mt. Mikaeli | Valeriana Mayagaya (MwanaSayuni)

Malaika watakatifu ni rafiki zetu na watumishi wetu. Tuwaheshimu, tuwapende, tukimbilie maombezi yao yenye nguvu kwa kusali rozari hii na sala zingine.

ROZARI/TASBIHI YA MT. MIKAELI
A. Penye Msalaba/medali, sali:
i) Ishara ya Msalaba
ii) K: Ee Mungu utuelekezee msaada:…… W: Ee Bwana utusaidie hima
iii) K: Atukuzwe Baba……… x1

B. Kwenye punji nne. Sali sala ya Baba yetu… kwa kila punje kama ifuatavyo:
Punji ya 1: Kwa heshima ya Mt. Mikaeli Malaika mkuu, Baba yetu……..
Punji ya 2: Kwa heshima ya Mt. Gabrieli Malaika mkuu, Baba yetu……
Punji ya 3: Kwa heshima ya Mt. Rafaeli Malaika mkuu, Baba yetu……
Punji ya 4: Kwa heshima ya Mt. Malaika mlinzi, Baba yetu……

C: Kwenye Mafungu
Salam na maombi kwa makundi ya Malaika…… kwa heshima ya makundi tisa ya Malaika.
1. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika Serafimu, Bwana awashe mioyoni mwetu moto wa mapendo kamili. Amina.. Baba yetu x1, Salaam Maria x3
2. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika Kerubimu, Bwana atuwezeshe kuacha njia mbaya na kuenenda katika njia ya ukamilifu wa kikristo. Amina.
Baba yetu x1, Salaam Maria x3
3. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika Wenye Enzi, Bwana atujalie roho ya unyofu na unyenyekevu wa kweli. Amina. Baba yetu x1, Salaam Maria x3.
4. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika Watawala, Bwana atujalie Neema ya kushinda maasi yote na tamaa mbaya. Amina. Baba yetu x1, Salaam Maria x3.
5. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika Wenye Nguvu, Bwana atukinge na vishawishi na mitego ya Shetani. Amina. Baba yetu x1, Salaam Maria x3.
6. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika wenye Mamlaka, Bwana atukinge na mwovu wala tusianguke kishawishini. Amina. Baba yetu x1, Salaam Maria x3.
7. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika Wenye mipango, Mungu atujalie roho ya utii wa kweli. Amina… Baba yetu x1, Salaam Maria x3.
8. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika Wakuu, Bwana atudumishe katika Imani na katika kazi zote njema ili tujaliwe utukufu wa milele. Amina… Baba yetu x1, Salaam Maria x3.
9. Kwa maombezi ya Mt. Mikaeli na ya kundi takatifu la Malaika, Bwana atujalie ulinzi wao hapa duniani na baadaye watuongoze kwenye furaha za mbinguni. Amina…


Ee Mtukufu Mt. Mikaeli, Mwana Mfalme na mkuu wa majeshi ya mbinguni, mlinzi wa roho, mshindaji wa pepo wabaya, mtumishi katika nyumba ya Mungu, mfalme na msimamizi wetu mstaajabivu, mwenye nguvu za juu na akili pendevu, utuokoe na maovu yote sisi tunaokutumainia na kwa ulinzi wako tuweze kumtumikia Mungu kila siku kwa uaminifu zaidi.
K: Utuombee Ee mtukufu Mt. Mikaeli mkuu wa kanisa la Yesu Kristo;
W: Ili tustahili kupata ahadi za Kristo.
Tuombe:
Ee Mungu Mwenyezi wa Milele, kwa wema na huruma Yako ya ajabu, umetaka watu wote waokoke, ukamweka Malaika Mikaeli kuwa Mkuu wa kanisa lako, atukinge na adui zetu wasitusumbue saa ya kufa kwetu, bali tuongozwe naye kwenye utukufu Wako mkuu, tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Litania ya Mt. Mikaeli:

Комментарии

Информация по комментариям в разработке