Mashujaa vita vya Kagera wasimulia waliyopitia hadi kushinda

Описание к видео Mashujaa vita vya Kagera wasimulia waliyopitia hadi kushinda

Wakati Tanzania ikiadhimisha Siku ya Mashujaa leo Julai 25, 2024, mashujaa waliopigana vita vya Kagera dhidi ya utawala wa Idd Amin wa Uganda, wamesimulia walivyolipigania Taifa, huku wakiwahimiza vijana waliopo jeshini kufuata nyayo zao katika kulinda amani ya nchi.

Vita kati ya Tanzania na Uganda ilipigana mwaka 1978 hadi 1979 ikianzia katika Mkoa wa Kagera ambapo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana majeshi ya waasi wa Uganda, walimuondoa kiongozi wa kijeshi wa Uganda wakati huo, Idd Amin.

Maofisa wanne wastaafu wa JWTZ waliopigana kwenye vita hiyo wamesimulia ujumbe waliopewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakielekea vitani na namna walivyopigania amani na ushindi dhidi ya Amin.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке