Nahodha || Dodoma Adventist Chorus

Описание к видео Nahodha || Dodoma Adventist Chorus

NAHODHA
Siku moja Yesu aliwaambia
Wanafunzi wake hebu na tuvukeni ng'ambo
Wakapanda wote ndani ya chombo
Mara tufani chombo kikaanza kujaa maji
Wakati huo Yesu amelala
Wakamwendea kumwamsha
"Bwana Twaangamia"
Akasimama, kakemea upepo
kukawa shwari dhoruba zikakoma

Kisha akageuka
(Kisha akageuka)
Akawauliza
(Akawauliza)
Imani yenu i wapi
(Je imani yenu i wapi nao wakaogopa)
Ni nani huyu ambaye
(Je ni nani huyu ambaye)
Pepo na Bahari vinasikia sauti yake.

Huyu ni Nahodha mwenye uzoefu mkuu
Mikononi mwake chombo huwa salama.
Unawezamwamini maana Chombo hakijawahizama Akiwa ni Nahodha
Mambo yote huwa salama

Katikati ya Dhoruba na Shida
Pepo zivumapo na Bahari ichafukapo
Unaweza kudhani amelala
Na hajali kuhusu shida zote upitiazo
"Je ni kweli huyu ndiye ambaye
Alisema 'takuwa nami Tena nisiogope
Nina mashaka na uwezo wake
Je ni kweli anaweza kuokoa?"

Usiogope ndugu
(Usiogope ndugu)
Na usifadhaike
(Na usifadhaike)
Imani yako weka kwake (hajawahi kushindwa)
Nahodha huyu si mwingine
Bali Bwana Yesu, amini utafika salama

Huyu ni Nahodha..

Huyu ni Nahodha mwenye uzoefu mkuu
Mikononi mwake chombo huwa salama.
Unawezamwamini maana Chombo hakijawahizama Akiwa ni Nahodha
Mambo yote huwa salama

Mambo huwa ni salama Bwana Yesu akiwa ni Nahodha

Huyu ni Nahodha mwenye uzoefu mkuu
(Mikononi mwake)
Mikononi mwake chombo huwa salama.
(Usiwe na shaka)
Unawezamwamini maana chombo hakijawahizama Akiwa ni Nahodha
(Akiwa ni Nahodha..)
Mambo yote huwa salama
(Bwana akiwa chomboni)
Mambo yote huwa salama
(Weka tumaini lako kwake)
Mambo yote huwa salama.


Luka 8:22-25
[22]Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.
[23]Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
[24]Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.
[25]Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?

Artist: Dodoma Adventist Chorus
Song Title: Nahodha
Audio Mixing and mastering: Job Music
Video: RJ Studio (Mr RJ)

Email: [email protected]

CONTACTS
+255 746 698 570
+255 622 309 142

You can also find us on:
https://audiomack.com/dodomaadventist...

Instagram
  / dodomaadventistchorus  

and all other digital platforms for audio.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке