WITO WA KUUJUA WAKATI SEH: III

Описание к видео WITO WA KUUJUA WAKATI SEH: III

Tunaishi katika miisho ya dunia hii, somo hili la WITO WA KUUJUA WAKATI SEH: III ni uchambuzi wa matukio ya siku za mwisho katika unabii ili kuyaweka wazi yaliyotabiriwa kama dalili na ishara za ukaribu wa kurudi kwa Yesu. Ndipo tukiyajua hayo, tutakuwa na akili za kizijua nyakati na akili za kujua nini tunapaswa kutenda kwa sasa, kama ilivyokuwa nyakati za Wana wa Isakari, kwa maana Wana wa Isakari wanahitajika pia kwa wakati huu na wanapatikana pia katika Kanisa la Mungu. Somo hili linakufikia kama matokeo ya kuzingatia agizo la Bwana katika roho ya unabii, kwa maana nabii Ellen G. White anasema hivi; “Wakati ulimwengu wa Kiprotestanti kwa mtazamo wake unafanya makubaliano na Rumi, hebu tuamke na kuelewa hali na kuona mashindano yaliyo mbele yetu katika uhalisia wake. Hebu walinzi sasa wapaze sauti zao na kutoa ujumbe ambao ni ukweli wa wakati huu. Hebu tuwaonyeshe watu wapi tumefika katika historia ya kinabii na tutafute kuamsha roho ya Uprotestanti wa kweli……...” {5T 716.2}. Kwa kweli, uprotestanti umeshafanya makubaliano na Rumi na hivi karibuni sheria ya jumapili itapitishwa nchini Marekani. Kwa sababu hiyo basi, huu ndio wakati wenyewe hasa wa kuitikia wito wa Bwana katika nukuu hapo juu. Kama matokeo ya muitikio huo, somo hili linakufikia. Bwana Yu nawe na endelea kubarikiwa unapofuatilia masomo haya.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке