Zembwela Afunguka Ukweli Wote Mpaka Kuacha Kazi East Africa | SALAMA NA ZEMBWELA PART 1

Описание к видео Zembwela Afunguka Ukweli Wote Mpaka Kuacha Kazi East Africa | SALAMA NA ZEMBWELA PART 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

MSAFIRI HUFIKIRI

Moja ya jambo ambalo nimejifunza kuhusu maisha na kufanikiwa ni KUTOKATA TAMAA wakati unatafuta ila kubwa kuliko ni wajibu wetu kutojiona tuko JUU zaidi ya wengine na kuamini kwamba pale ulipo hakuna siku ambayo utakuja KUTETEREKA. Katika makosa ambayo unaweza kuyafanya ni kuamini hilo jambo KUBWA.

Hillary Daudi ni Kaka yangu na Rafiki yangu, mimi nilianza kwa kumuona yeye kwenye TV kabla sijakutana naye rasmi kwenye mwanzo kwa miaka ya 2013 kupitia Rafiki yangu mwengine aneyeitwa Mussa Hussein, Mussa na Zembwela ni washkaji ambao wali click tu mara ya kwanza walivyoonana na Mussa alipomsikia tu Zembwela aliona atamfaa sana kama atakua partner wake kwenye kile kipindi alichokua akifanya cha kuanzia saa tatu asubuhi pale EA Radio.

Zembwela alikua mmoja wa waanzilishi wa kipindi cha vichekesho pale ITV akiwa na Rafiki yake Marehemu Max, na jambo ambalo mimi nilikua silijui ni kwamba Zembwela yeye ndiye aliyekua muandishi wa yale maigizo mafupi mafupi waliyokua wanafanya, na hilo swali nilimuuliza baada ya kusikia tetesi mtaani kwamba toka Max atangulie mbele ya haki yeye Zembwela amepoteza kabisa ile ladha na kwamba sasa si yule wa zamani. Ki kawaida tu kwanza hawezi kuwa kama yule wa zamani na zaidi ni kweli ladha pengine lazima ipotee maana sasa hivi yuko peke yake, ila je kipaji? Binafsi nadhani Zembwela ana kipaji na utashi wa hali ya juu ambao unamfanya aendelee kuwepo pale alipo na sasa akiwa anasimama kama Ndimu kwenye Radio ya Wasafi FM pale asubuhi anapokua anachambua magazeti.

Mwanzo nilikuambia Zembwela alianzia EA Radio baada ya kuvutwa na Mussa pale, na alikaa kwa kipindi hata baada ya Mussa kuondoka yeye aliendelea kuzungusha gurudumu la Super Mix ila baadae mambo yakabadilika na ikambidi aende kutafuta ustaarabu mwengine na sehemu nyengine. Maisha yako wakati mwengine yanaweza kukupeleka sehemu ambayo wala ulikua huitarajii.

Sasa pia amerudi kwenye TV na kaniibia siri pia kwamba hivi karibuni anatarajia kuanza series ambayo wao kama Wasafi TV wamekua wakiipika kwa kipindi sasa. Naamini hii itakua habari njema kwa wengi ambao wamekua wakiisubiria kwa hamu.
Na pia kasema itaanza hivi karibuni.
Mimi na Zembwela pia tumeongelea maisha yake binafsi, kuondoa kwa Max, kazi za kileo na mustakabali wa Siasa na wana Siasa na mengine tele. Moja kubwa ambalo naweza kukuahidi ni enjoyment na kucheka, hakika haya UTAYAPATA.

Tafadhali enjoy,
Love,
Salama.

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Комментарии

Информация по комментариям в разработке