KAULI YA WAZIRI NAPE ILIYOMPONZA HII HAPA |TUTASHINDA HATA KWA BAO LA MKONO

Описание к видео KAULI YA WAZIRI NAPE ILIYOMPONZA HII HAPA |TUTASHINDA HATA KWA BAO LA MKONO

Nape ameonesha uchanga (immaturity) kuzima akaunti yake ya X /Twitter.

Baada ya kutenguliwa nafasi ya uwaziri, Nape Nnauye amesusa kutumia mtandao wa X, zamani ukijulikana kama Twitter.

Yawezekana ameamua kupumzika kwa muda ili kuepuka zogo kutoka kwa vijana makini na hata vijana wa hovyo wanaomshambulia kila siku. Naam, Nape hushambuliwa sana kwa sababu ya kauli zake zenye utata, pamoja na tabia zake za kiburi na jeuri anazoonesha kwa watu.

Kwanini Nape Nnauye azime akaunti ya X?
Kwa maoni yangu, uchanga wa kifikra ndio umemfanya afanye hivyo. Naam, ni uchanga. Immaturity.

Kwa tafsiri ya haraka, Nape Nnauye 'amesusa'. Sasa anamsusia nani? Anamsusia Rais aliyemtengua? Kwani ni yeye peke yake aliyetenguliwa? Nape aache utoto.

Ameshindwa kumshukuru Rais kwa muda aliyomteua kuwatumikia watanzania, badala yake amesusa.
Ameshindwa kumshukuru na kuonesha kukubaliana na maamuzi ya Rais, badala yake amesusa.
Ameshindwa kuahidi kuendelea kumsaidia Rais na mwenyekiti wake wa Chama kama mbunge wa kawaida, badala yake amesusa.
Nape anamsusia nani?
Hajui kama kususa kunaweza kumfanya asirudi tena? Anamsusia Mswahili wa Zanzibar? Tena Makunduchi?
Nape acha utoto!

Комментарии

Информация по комментариям в разработке