Angel Benard - Mwanzo (Official Music Video)

Описание к видео Angel Benard - Mwanzo (Official Music Video)

Upana wa Mungu hauwezi kuelezeka. Katika miaka ya kuishi maisha ya imani nimejifunza jambo moja, sijui mengi kama nilivyodhani wakati Nina umri wa mwaka mmoja katika imani. Hatujui Kama tunavyodhani, hatumjui kama tunavyodhani. Mungu ni Mpana sana na njia zake zipo juu mno kuliko njia zetu. Anaweza fanya lolote lile, kwa namna yoyote ile, wakati wowote ule, kupitia mtu yeyote yule.

Yeye ni mwanzo kabla ya mwanzo tunaodhani tunaujua (Mwanzo 1:1) na ni mwisho baada ya mwisho tunaodhani tunaujua pia (Ufunuo).

Hakuna hata mmoja wetu ambae anahaki ya kumkatia Mungu tamaa. Mambo yote yatapita ila Mungu anabaki wa kuaminika. Kila kitu kitapita isipokuwa neno lililotoka katika kinywa cha Mungu.

Nakuombea usiyadharau mambo mapumbavu maana nayo hutumiwa kuthibitisha ukuu wa Mungu. Usidharau njia za Mungu au kuzichukia. Hatujui yote, na yeye ndio yote katika yote. Nakuombea urudishe na udumishe imani kwa Mungu, hatakuangusha. HAJAWAHI KUTUANGUSHA HATA PALE WANADAMU WANAPOKUANGUSHA.

Muamini mwanzo kabla ya mwanzo na mwisho kabla ya mwisho kuliko mazingira, hisia na hofu. Bwana ni wa KUAMINIKA.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке