TUTAISHIA KUSEMA (OFFICIAL VIDEO) - Kwaya Kuu Mt. Cesilia Arusha Tanzania

Описание к видео TUTAISHIA KUSEMA (OFFICIAL VIDEO) - Kwaya Kuu Mt. Cesilia Arusha Tanzania

Download or listen online: https://mdundo.com/song/2161772

Performers: Kwaya Kuu Mt. Cesilia Arusha Tanzania
Publisher: Verony Productions Ltd.
Copyright ©Verony Productions Ltd.

MTUNZI: F. Bukene

Tutaishia kusema hii dunia mbaya (kweli) * 2
Mungu kaikamilisha bila kusahau kitu sasa
Dunia iweje mbaya kwa sababu ya walimwengu

Mungu kaumba dunia kwa mpango kamilifu
Kuhakikisha usalama kwa kila alichokiumba
Mazao yanastawi chakula kinatutosha, na mvua
zinanyesha sana kwa sababu ya upendo wake.

Wapo walio fukara ambao hawajiwezi
Matajiri hawawasaidii japo wana uwezo
Pia mahospitalini hongo zimeshatawala
Pesa sasa zinatawala kuliko upendo wa Mungu.

Viongozi maofisini wananyanyasa raia
Bila hongo hakuna kazi ubinadamu uko wapi
Dunia hii ya leo imetapakaa damu
Silaha za kutisha sana kutwa kucha zafanya kazi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке