LIVE ▶ | IBADA YA TATU | JUMAPILI | 19 / 05 / 2024

Описание к видео LIVE ▶ | IBADA YA TATU | JUMAPILI | 19 / 05 / 2024

Siku ya kukumbuka kushuka kwa Roho Mtakatifu ( Pentekoste)

SOMO: ROHO MTAKATIFU NGUVU YETU
Yohana 20: 19 - 23

MHUBIRI: MCH. CHARLES MZINGA
..................
ZABURI 143: 1 - 12
1. Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu Unijibu Kwa uaminifu wako, Unijibu kwa haki yako.
2. Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.
3. Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani.
4. Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umeshtuka.
5. Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako.
6. Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.
7. Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
8. Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.
9. Ee BWANA, uniponye kutoka kwa adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche.
10. Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa,
11. Ee BWANA, uniponye kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;
12. Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.

WAEFESO 1: 13 - 14
13. Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, Habari Njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa mhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
14. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

YOHANA 20: 19 - 23
19. Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
20. Naye akiisha kusema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.
21. Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.
22. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
23. Na wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

.............
👇👇👇
// NAMBA ZA SADAKA //
▶ LIPA KWA [ M-PESA ] - 579 579 4
▶ NAMBA YA MPESA - 0757 - 391 - 174
JINA: KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

▶ MAENDELEO BANK
A/C NO 0137 9274 6021
JINA: LUTHERAN CHURCH AZANIA FRONT CATHEDRAL

TUFUATILIE KWENYE MITANDAO KWA TAHARIFA ZAIDI:
Instagram page:
/ kkkt_azaniafront_cathedral
Website: https://www.azaniafront.org/
Facebook:
/ kkkt-azania-front-cathedral-101434162039079
#azaniafrontcathedral #ibada #lunchhour #morningglory #sundayservice #lutheran

Комментарии

Информация по комментариям в разработке