RUSSIA YADUNGUA NDEGE YA UKRAINE AINA YA MiG29, BLINKEN AIKAYIA TAMAA

Описание к видео RUSSIA YADUNGUA NDEGE YA UKRAINE AINA YA MiG29, BLINKEN AIKAYIA TAMAA

Moscow. Vikosi vya Russia vimedungua ndege ya kivita ya Ukraine aina ya MiG-29. Taarifa ya kudunguliwa ndege hiyo imetolewa leo Jumapili Januari 5,2025, na Wizara ya Ulinzi ya Russia.

Wizara hiyo imesema vikosi vya Ukraine pia vimepoteza makombora kadhaa yaliyotengenezwa katika mataifa ya magharibi ikiwemo gari ya kivita aina ya Bradley.

“Mashambulizi 17 yaliyorushwa na adui yetu Ukraine yamedhibitiwa. Vikosi vyao vimepoteza zaidi ya wanajeshi 410, vifaru viwili aina ya Leopards vilivyotengenezwa Ujerumani, gari la kurushia makombora, na magari matatu ya kubeba wanajeshi ikiwemo gari aina ya M113 iliyotengenezwa Marekani,” taarifa hiyo imesema kutokea Mkoa wa Donetsk unaoshikiliwa na vikosi vya Russia.

Ukraine pia imepoteza kombora aina ya L-119 lenye kipenyo cha milimita 105 lililotengenezwa nchini Uingereza,” imesema taarifa ya Wizara hiyo.

Tovuti ya Russia Today, imeripoti kuwa katika moja ya kambi, Ukraine imepoteza wanajeshi 230 katika mashambulizi ya kushtukiza yaliyofanywa mapema leo Januari 5,2024 na vikosi vya Russia.

İdadi kubwa ya ndege za Kisovieti aina ya MiG-29 zimepelekwa Kiev nchini Ukraine na washirika wake ambao ni kutoka mataifa ya Jumuiya ya Ulaya tangu Februari 2022, Russia ilipotangaza kuanza Operesheni zake za kijeshi nchini humo.

Tovuti hiyo pia iliripoti kuwa Poland iliipatia Ukraine ndege kadhaa za kivita za Kisovieti mwaka 2023, hata hivyo, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Poland, Pawel Zalewski alisema ndege za kivita aina ya F-35 zilizotengenezwa nchini Marekani utakuwa mbadala wa ndege hizo.

Hata hivyo, Desemba 2024, Zalewski alisema Poland haitopeleka ndege zake za kivita zilizobaki nchini Ukraine ili kutohatarisha usalama wake.

Hadi sasa Marekani na Umoja wa Ulaya umeshaipatia Ukraine misaada ya kijeshi, Kifedha na silaha inayokadiriwa kufikia Dola za Marekani bilioni 100 tangu kuanza kwa mzozo huo Februari 2022, huku yakisisitiza kuwa yanatoa msaada huo siyo kwa lengo la kuchochea mzozo huo.
Imeandaliwa na Mgongo Kaitira

Комментарии

Информация по комментариям в разработке