Salama Na Fid Q Ep 7 | NGOSHA WA MBASA Part 1

Описание к видео Salama Na Fid Q Ep 7 | NGOSHA WA MBASA Part 1

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast

Listen our Podcast on


‪Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬

‪ApplePodcasts Link https://apple.co/2Ou1bru‬

‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

NGOSHA WA MBASA
Nakumbuka kipindi ambacho Fidi alikua anaamini kabisa kama kuweka ‘uso wa mbuzi’ ndo kulikua kunakufanya uwe ‘hard core’, sina uhakika lini aliachana na dhana hiyo ila kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi tabasamu na bashasha vimekua havibanduki kwenye uso wake, jambo ambalo mimi kama rafiki nalifurahia sana. Nakumbuka baadhi ya marafiki zangu wa kike ambao ni wapenzi haswa wa mziki wake walikua wakiniambia eh, sema rafiki yako mgumu jamani, Kha! Mi hucheka tu na baadae wakishazoeana basi sidhani kama kuna hata mmoja anaweza kusema kitu kibaya kuhusu yeye. Nilikua nacheka kwasababu mimi naamini namfahamu rafiki yangu huyu, yeye hupenda sana matani, na kucheka na marafiki wa karibu wanaweza wakathibitisha hilo maana katika watu ambao unaweza ukawatania weeee mpaka asubuhi, na utani mpaka wa vitu vyengine ambavyo wewe wa karibu unaweza kusema ey, hiyo sasa imepitiliza, yeye waala... Atacheka tu!

Mwenye kipaji chake cha kujifunza mwenyewe, nasema hivyo kwasababu nadhani kufahamiana kwetu na kuelewana kwetu pia kunatokana na kuwa na vitu vinavyofanana ndani yetu. Kajifunza jinsi ya kupenda kusoma vitabu mwenyewe, kujifunza jinsi ya kuandika na kurap mwenyewe, kajiendeleza mwenyewe (bila ya shaka kuna watu walomsaidia kwa tafu za hapa na pale ila walitokea baada ya kuona jitihada zake). Alihakikisha anasafiri kwenda nje ya nchi na Africa kwa jitihada zake mwenyewe na mpaka leo, kukiitwa watu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha Hip Hop ya nyumbani hapa ilipo basi jina lake litakua ni miungoni ya yale yatakayopata heshima ya juu kabisa. Pia anachekesha sana. Uelewa wake wa baadhi ya vitu unaweza ukakuacha mdomo wazi wakati mwengine. Kwenye uwepo wake? Vicheko lazima vitawale.

Hii siku nilitia nae story haikua kama kazi, bali kama mtu na rafikiye tu wakitia story juu ya njia za maisha ambazo tumepitia mpaka sasa. Fidi amekuzwa na Mama yake ambae alikua ni mfanyakazi wa serikalini (ameshastaafu), alikulia mkoani kama wengi wetu, alifika Dar akakaa kwa ndugu kama wengi wetu, alianzia sehemu na kutoka hapo mdogomdogo akajijenga kufikia hapa alipo. Humu tumeongelea hayo, watoto, muziki, ndoa, maisha ya wasanii na maendeleo kwa ujumla. Yangu matumaini uta enjoy na kuelewa baadhi ya vitu zaidi na zaidi.

Here’s to Ngosha wa Mbasa.

Love,
Salama.
Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Комментарии

Информация по комментариям в разработке