MUONEKANO WA ENEO LAUTEKELEZAJI WA MRADIWA BONDE MSIMBAZI

Описание к видео MUONEKANO WA ENEO LAUTEKELEZAJI WA MRADIWA BONDE MSIMBAZI

MUONEKANO WA ENEO LA
UTEKELEZAJI WA MRADI
WA BONDE MSIMBAZI

Serikali ya Tanzania, kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (PO-RALG) kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, inatekeleza Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 260, ambapo kiasi cha dola 200 ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia, dola milioni 30 ufadhili wa Serikali ya Uholanzi na dola milioni 30 ni mkopo kutoka Serikali ya Hispania.

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania (TARURA) na Wakala ya Barabara za Taifa Tanzania (TANROADS) ndiyo watekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi kwa niaba ya wizara husika.

Lengo kuu la Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi ni kukabiliana na mafuriko pamoja na kuimarisha mipango miji na uendelezaji wake katika eneo la chini la Bonde la Msimbazi, ambalo lina fursa kubwa za kiuchumi kwa jiografia yake ya kuwa katikati ya Jiji.

OR-TAMISEMI kupitia TARURA ni mtekelezaji mkuu wa mradi, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kazi zote za mradi, isipokuwa ujenzi wa daraja la Jangwani, ambalo litajengwa na TANROADS. Muda wa utekelezaji wa mradi ni miaka sita (6) 2022-2028.

Zoezi la kulipa fidia kwa waathirika wa mradi limefanyika kwa umakini mkubwa ambapo mpaka kufikia Agost 12, 2024, jumla shilingi bilioni 64.9 zimeshalipwa kama fidia ya mali kwa waathirika 2,533; bilioni 8.1 zimelipwa kwa ajili ya kupata ardhi mbadala kwa waathirika 2,042 na shilingi milioni 30.7 zimeliplwa kama posho ya pango na usafiri.

Kazi zitakazotekelezwa katika Mradi ni pamoja na: -
• Ulipaji wa fidia kwa wakazi
• Ujenzi wa miundombinu
• Ujenzi wa karakana ya mabasi ya mwendokasi
• Ujenzi wa daraja la kisasa Magomeni (400m)
• Upanuzi na ujenzi wa kingo za mto Msimbazi
• Ujenzi wa Soko
• Udhibiti wa taka ngumu
• Ujenzi wa bustani ya Jiji pamoja na kuendeleza maeneo ya makazi na biashara
• Kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi
• Kurejesha ustawi kwa jamii (livelihood restoration)
• Usimamizi wa bonde

Комментарии

Информация по комментариям в разработке