Ndege ya kwanza kutengenezwa Tanzania yaanza safari zake

Описание к видео Ndege ya kwanza kutengenezwa Tanzania yaanza safari zake

Ndege ya kwanza kutengenezwa Tanzania, aina ya Skyleader 600, sasa ipo tayari kufanya safari zake mbalimbali nchini na nje ya nchi. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa AAL, David Grolig, wakati wa safari yake ya kwanza ambayo imefanyika mapema leoJumapili September 29, 2024, ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kuondoka mkoani Morogoro.

Grolig amesema ndege hiyo ina ubora wa juu, hivyo imepewa kibali cha kuanza safari zake nchini.
"Tulifanya utafiti wa kina ili kuelewa mahitaji ya wasafiri wa kibiashara, ambao mara nyingi hufanya safari za umbali mrefu. Kutokana na utafiti huo, tumeamua kutengeneza ndege hii ili kuwasaidia wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi zaidi na kuhudhuria mikutano mbalimbali," amesema Grolig.

AAL ni kampuni ya kwanza nchini Tanzania kutengeneza ndege za aina hii, ambazo zina matumizi ya kibiashara na binafsi. Mwaka ujao 2025, kampuni hiyo inatarajia kuzindua Skyleader 500, ndege ya gharama nafuu itakayotumika katika shughuli za kilimo na nyingine zinazohusiana na maendeleo ya vijijini.

Grolig aliongeza kuwa kampuni hiyo inafanya kazi na timu ya wafanyakazi wa Kitanzania na Kicheki (Jmhuri ya Czech), na pia imewapatia fursa za ajira vijana wa Kitanzania. Baadhi ya wafanyakazi hao wamechaguliwa kufanya mafunzo kwa vitendo katika Jamhuri ya Czech, kuongeza ujuzi wao katika tasnia ya ndege.

Hii ni hatua muhimu katika maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga nchini Tanzania, ikionyesha uwezo wa ndani katika kutengeneza vifaa vya kisasa vya usafiri.

Video na KHATIBU MGEJA.




























































#samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #alahlytv #alahlysc #miraj

Комментарии

Информация по комментариям в разработке