MAFANIKIO MIAKA 60 YA UHURU, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba, Mkuu wa Chuo TMA Monduli Aelezea Mip

Описание к видео MAFANIKIO MIAKA 60 YA UHURU, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba, Mkuu wa Chuo TMA Monduli Aelezea Mip

TANZANIA MILITARY ACADEMY (TMA) TUMEPIGA HATUA KUBWA¬
Kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Chuo ambacho kinafundisha Maafisa wanafunzi wa JWTZ, Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba anaelezea Mafanikio yaliyofikiwa na Chuo hicho hivi sasa.

Akizungumza wakati wa Mahojiano maalumu ya Mafanikio ya Miaka 60 ya Uhuru, Brigedia Jenerali Mwaseba anasema Jeshi Kupitia TMA linajivunia kuwafundisha na kuwaandaa Maafisa Wanafunzi katika weledi wa hali ya juu Kijeshi ili kukidhi mahitajio ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Aidha, Mkuu wa Chuo hicho anaelezea Mafanikio ya Chuo katika kumudu kufundisha Kozi mbili kwa wakati mmoja CORE MODULES inayohusu kufundisha masomo yote ya Kijeshi kwa kuendesha Kozi ya Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi pamoja na masomo ya kiraia FUNDAMENTAL MODULES ambapo Chuo hicho kinashirikiana na Taasisi zingine za kiraia kama Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) pamoja na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Jijini Arusha.

Hata hivyo, Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema mipango ya baaaye ni kukifanya Chuo cha TMA kuwa Chuo Kikuu.


Maelezo zaidi kuhusu mahojiano haya tufuatilie kupitia YouTube Channel yetu ULINZI CHANNEL,

Tufuatilie pia kwenye mitandao ya kijamii Instagram, Facebook na Twitter kwa Jina moja tu Wizara ya Ulinzi na JKT

Waweza kupata taarifa zetu pia kupitia website yetu www.modans.go.tz

Комментарии

Информация по комментариям в разработке