MAZINGE AWAASA WAISLAM KUTUNZA SABATO: MDAHALO, SIKU YA TAKATIFU YA IBADA ILIYOAGIZWA NA MUNGU

Описание к видео MAZINGE AWAASA WAISLAM KUTUNZA SABATO: MDAHALO, SIKU YA TAKATIFU YA IBADA ILIYOAGIZWA NA MUNGU

Mdahalo uliofanyika Tanga Tarehe 2 Hadi 3 Feb. 2023. Vitabu vyote vinathibitisha kwamba, siku pekee aliyoagiza Mwenyezi Mungu kufanyika ibada takatifu ni siku ya Sabato-Jumamosi.

Historia inathibitisha kwama Siku ya Ijumaa haikuwa siku rasmi ya ibada katika Uislam. Siku hii ilianzishwa na Waislam wa Madina (Answar) kabla hata Muhammad hajahamia huko (Hijra). Lengo lao lilikuwa ni kujitofautisha na Wayahudi na Wakristo. Muhammad alipo hamia Madini alikuta waislam wa huko wanakusanyika katika siku ya Ijumaa. Siku moja siku ya Ijumaa, Muhammad akiwa anahutubia msikitini, msafara wa wafanya biashara wakaingia mjini kutoka sham, kukawa na vurugu na kelele za wafanya biashara. Masahaba wote wakakimbia kwenda huko na kumwacha anahudubia wakabaki watu 12 tu! Hapo ndipo ikashuka sura ya Ijumaa katika Qur'an kwa lengo la kuwafanya watu waache mambo ya biashara wakati wa Ibada unapokuwa umefika.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке