Pd Kamugisha Awasili DSM/Vicheko vyatawala Parokia ya Kilongawima/Karama aliyo nayo siyo ya kawaida.

Описание к видео Pd Kamugisha Awasili DSM/Vicheko vyatawala Parokia ya Kilongawima/Karama aliyo nayo siyo ya kawaida.

Tarehe 01 November 2021 Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu katoliki la Dar Es Salaam Mhasham Henry Mchamungu Aliongoza Ibada ya Uzinduzi wa Wiki mbili za Neema katika Parokia ya Mtakatifu kizito Kilongawima Mbezi Jijini Dar Es salaam Ambapo alimpongeza Paroko wa Parokia hiyo Padre Mukandala kwa maandalizi mazuri ya kuwalisha neno la Mungu waamini wa Parokia yake kwa kuwakusanya zaidi ya Mapadre 15 kutoka majimbo mbalimbali ya Tanzania ambao ndio watakaotoa Mafunzo kwa waamini hao.

Semina hiyo ya wiki mbili za Neema imeanza kurindima tarehe 02/11/2021 katika viwanja vya Parokia hiyo na Miongoni mwa Mapadre ambao wamekuwa wa kwanza kabisa kutoa mafundisho ni Padre Novatus Mbaula kutoka Msimbazi Centre Dar es salaam huku akifuatiwa na Padre Faustine Kamugisha kutoka Parokia ya Minziro jimbo katoliki la Bukoba.

Waamini wengi waliofika katika Siku ya kwanza ya mafundisho hayo wengi wao wameonekana kujawa na Tabasamu mwanana mara baada ya Wakufunzi hao kuwalisha Chakula cha kiroho huku wengi wao wakieleza kuwa, ni wazi wale ambao hawajashiriki wanakosa mengi ikiwemo faraja ya kweli ambayo inawarudisha katika imani dhabiti pamoja na kuimarika zaidi ndani ya Ubatizo wao.

pata nafasi ya kutazama video hii na kuwa miongoni mwa wale ambao wamefuatilia Mubashara.
#BreezOnlineTv​​​​​​​​​​​​​ #Kilongawima
Breez Online Tv
S.L.P 38655
Dar Es Salaam Tanzania
Phone No: +255 756494796
Barua pepe: [email protected]

Mitandao Mingine ya Kijamii:
Facebook: breez online Tv
Facebook Link:   / breez-online.  .
Instagram:Breez Online Tv

Комментарии

Информация по комментариям в разработке