MASHUHUDA WA AJALI YA ASKOFU SENDORO WASIMULIA TUKIO ILIVYOTOKEA

Описание к видео MASHUHUDA WA AJALI YA ASKOFU SENDORO WASIMULIA TUKIO ILIVYOTOKEA

Mwanga. Mmoja wa madereva wa lori, Athuman Jumanne amesimulia namna ajali ilivyotokea huku akisema dereva wa gari dogo aina ya toyota Prado lililokuwa likiendeshwa na Askofu Sendoro, lilitaka kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele hivyo kusababisha ajali.

Alisema, baada ya kutokea ajali walikuja wasamaria wema kutoa msaada eneo la tukio na wakati wanaondolewa eneo la tukio aliyekuwa kwenye gari dogo(Askofu Sendoro) alikuwa ameshafariki dunia.

Mark Antony, ambaye ni miongoni mwa madereva waliopata ajali eneo hilo la tukio, amesema muda mfupi baada ya gari lililokuwa likiendeshwa na Askofu Sendoro kuyapita magari mengine lilipinduka baada ya kugongana uso kwa uso na gari lililokuwa likitokea Mwanga kuja njia panda ya Himo, Moshi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке